watu walio tembelea leo

Rais Kikwete aongoza shughuli za kuagwa kwa marehemu Kapteni John Komba

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete Jumatatu hii ameongoza shughuli za kuagwa kwa aliyekuwa mbunge wa Mbinga na muimbaji mahiri, Kapteni John Komba aliyefariki Jumamosi iliyopita. Shughuli hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa juu wa nchini. Baada ya shughuli ya kumuauga, mwili wake utasafirishwa kwenda wilayani Mbinga, Ruvuma kwa maziko siku ya Leo Jumanne.
Kifo cha Marehemu Komba kinakuwa ni pigo kubwa katika tasnia ya Burudani kutokana na mchango wake.
Marehemu John Komba alifariki dunia kutokana na tatizo la shinikizo la damu ambapo siku hiyo alizidiwa kutokana na sukari kushuka na kupelekwa katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.
Marehemu Kaptain Komba alizaliwa Marchi 18 mwaka 1945 alipata elimu ya msingi huko nchini Tanzania katika shule ya Lituhi baadae elimu ya sekondari katika shule ya sekondari ya Songea iliyopo kusini mwa Tanzania kuanzia 1971 hadi mwaka 1974.
Mwaka 1975 hadi mwaka 1976 Marehemu John Komba alijiunga na chuo cha ualimu kilichopo Kleruu Iringa, Kusini Magharibi mwa Tanzania ambapo alihitimu cheti cha ualimu.
Marehemu John Komba ni mwanajeshi ambaye alipata mafunzo ya uafisa wa Jeshi katika chuo cha Maafisa wa Jeshi kilichopo Monduli kaskazini mwa Tanzania mwaka 1978 hadi mwaka 1978.
Keptain John Komba pia alipata mafunzo mengine ya siasa kutoka chuo Kikuu cha Washngton International ambapo alitunukiwa shahada ya siasa mwaka 2006 hadi mwaka 2008.