Team Up date Sarah akipiga stories na Mbunifu wa mavazi kutoka Tanzania Sheria Ngowi
Sheria Ngowi ni kijana ambaye, mara chache sana unaweza ukakutana nae sehemu zile za bata, bars, night clubs, muda mwingi hutumia nyumbani na kazini, saa 4:00 ofisini hadi saa 4:00 usiku.
Akipiga stories na #Teamupdate wa teamtz.com , Sheria Ngowi ameongea vitu vingi ambavyo ni vizuri kwa kijana yeyote ambaye angependa kufanikiwa katika maisha yake.
Stories hii tunaiita Sheria Ngowi Part I, kila siku tutaendelea nae akiwa anafunguka vitu vingi kuhusu maisha yake na vitu mbalimbali ambavyo vitakujenga kimawazo uwe kijana, mzee au mtoto.
Akipiga stories na teamtz.com Sheria Ngowi ameongelea kuhusu kujenga kiwanda chake huko Bagamoyo jijini Dar es salaam, kufungua Sheria Ngowi TV ambayo itakuwa ikionyesha fashion and life style na channel ya Sheria. Ikianza kwa online na baadae kuwa TV rasmi ambayo itakuwa ikipatikana kwenye ving’amuzi.
Pia magari ya kubebea maharusi yanakuja, vile vile watahama kutoka Masaki watahamia kwenye Makao Makuu ya bidhaa zake (brand hq) atakapopata sehemu na mipango mengine mingi inakuja.
Alipoulizwa alipataje fursa ya kuwavalisha Marais mbalimbali, Sheria Ngowi alisema “hiyo ipo private kidogo, ila unajua kizuri kinajiuza na ni ubora tu wa kazi, bidii, tabia njema na kujiheshimu ndo siri ya mafanikio yote hayo”,
Kuhusu ni mbunifu gani ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania maybe angependa kufanya nae kazi, Sheria Ngowi amesema ni yeyote Yule ambaye anajiamini. Akimuongelea mwanamitindo Millen Magese na Flaviana Matata amesema wale ni watu ambao wanajianadaa, wanajiamini ndo maana wamefika hapo walipo, amesema kwa hawa ambao wapo hapa nyumbani hawana tofauti kubwa sana, tofauti yao ni kujiamini na kujielezea na kujituma sana muda wao wote wameweka kwenye kile wanachokifanya kwa sababu ile ndiyo ajira yao, hakuna kitu kingine hiyo ndio siri.
Mwaka jana alimvalisha Diamond kwenye tuzo za MTV, Je utaratibu unakuwaje labda msanii akitaka amvalishe? “utaratibu ni kama utaratibu mwingine, ni mtu binafsi kujiamini, mtu binafsi kujua nini anachokitaka, mtu binafsi kujua kwamba yuko tayari kubadilika, anajijua” alisema Sheria Ngowi.