watu walio tembelea leo

Profesa J: Nimefanya collabo na Chameleone kudumisha uhusiano!


Proffesor-Jay-akiwa-na-Jose-Chameleon-katika-hotel-ya-Southern-Sun-Dar-Es-Salaam  (1)
Profesa Jay amesema lengo la kumshirikisha Jose Chameleone kwa mara ya pili kwenye wimbo wake ‘Kwaajili Yako’ ni kuendelea kudumisha uhusiano wa wasanii wa Afrika Mashariki. Wawili hao wamewahi kufanya ngoma nyingine miaka kadhaa iliyopita iitwayo ‘Ndivyo Sivyo’.
“Tumekuwa wasanii ambao tunaweza tukaunganisha nchi zetu na sasa hivi tumekuwa na kilio kwamba East Afrika iwe pamoja,” amesema rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule.
“Tumeona tukimtumia Profesa J ambaye ni artist ambaye ni mkubwa hapa Tanzania na Jose Chameleone ni artist mkubwa yupo Uganda tunaweza tukatengeneza kitu kinaweza kikawa kina maana kubwa sana kwa wananchi wa Afrika Mashariki,” aliongeza.
Profesa amesema video ya wimbo itafanyika Uganda au Afrika Kusini.