watu walio tembelea leo

MITOTO YA GOLA HEWANI !



PICHA KUSHOTO NI KIONGOZI WA WATU WA GOLA BATAROKOTA NA KULIA NI BIG D

Kundi la muziki wa Bongo Fleva la jijini Mwanza lenye maskani yake Igoma, maarufu kwa jina la Watu wa Gola limekamirisha maandalizi ya video ya wimbo wao wa pili uitwao `mitoto ya gola`

Watu wa Gola ni kundi linaloundwa na wasanii wawili Paskal linda a.k.a Batarokota na Juma Hassan a.k.a Big D. Akionge  meneja wa Watu wa Gola linda Sangudi alisema songi Mitoto ya Gola imerekodiwa  katika studio ya M.O Records iliyopo jijini Mwanza chini ya mtarishaji Q the Don na video itafanyiwa na kampuni ya Kadide chini ya M.O. Records ambapo hadi wakati huu maandalizi yote yamekamilika .Gharama za kazi hii zimechangiwa na michango toka kwa wafadhiri mbalimbali wa jijini Mwanza wakiwemo Huruma Chirdren Centre ya Nyamhongolo na Zari Music and Entertment iliyopo Igoma jijini Mwanza ambao ndio wadhamini wakuu wa video ya wimbo `Mitoto ya Gola`.