watu walio tembelea leo

Batarokota: Bado nipo nipo kwenye ‘Asilia’


Pichani juu kutoka kushoto msanii Batarokota akiwa na aliyekuwa kocha wa Taifa Star na Yanga African Mbrazili Maxio Maxima na kulia ni Stiini Shija akiwa katika picha ya pamoja jijini Mwanza 2007,

MKONGWE katika muziki wa Bongo Fleva na nyimbo asilia ya kitanzania , Batarokota, ameibuka na kudai kwamba muziki wa asili ya kitanzania haujamshinda hivyo ataendelea kuimba Bongo Fleva na mziki asilia kwa kuwa nyimbo zake hazipotoshi jamii.

“Baada ya kukaa vizuri ndani ya asili na kupata baadhi ya tuzo nimeona naweza kufanya Bongo Fleva kwa ajili ya kuelimisha jamii huku nikiendelea na asilia, cha msingi ni kufuata maadili ya pande zote mbili kwa kuwa sina wimbo wa kupotosha jamii.
“Kingine kinachonipa moyo ni kwamba washabiki wangu wananikubali sana awangalii naimba Bongo Fleva au nyimbo asili bali wanaangalia ubunifu wangu,” alifafanua zaidi Batarokota.
Batarokota  aliwahi kuimba na wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva na nyimbo asilia akiwemo, Mama Nyamoko, Teddy Kalanda, Bobo Sukari, Big D, Ngollo 2 na wengine wengi lakini pia aliingia katika muziki wa asilia ya kitanzania na kuwa kimya kwa muda mrefu kiasi kwamba mashabiki wake wakadhani ameachana nao.