
Steve Nyerere alisema, “Kwanza watu wafahamu mimi sio dalali, bali nipo karibu na hao watu kwa hiyo naweza kumsaidia mtu kununua gari, Linex alinifuata kwamba anataka gari kama langu basi nikamuunganisha kwa huyo dalali, lakini baada ya hapo sikumuona tena Linex na mambo yalipomshinda mbona alikuja kwangu akitaka nimsaidie tena, aliyemtapeli gari Linex ni dalali sio mimi”.
Steve nyerere pia alifunguka mipango yake ya kutaka kugombea Ubunge jimbo la kinondoni kwa tiketi ya chama cha CCM, na kuwaomba wana kinondoni na watanzania kwa ujumla kuwezesha afanikiwe kuchukua kiti hicho.
“Nime amua kugombea sababu nina uwezo wa uongozi, mimi ni mwana kinondoni, na nina mpango wa kuendeleza jimbo langu, tukuze elimu na maisha ya kawaida ya wana kinondoni”, alisema Nyerere.
Aliendelea kwa kusema yeye ni kijana hivyo uongozi wake utakuwa kama wa Obama, kwani vijana wengi wanauwezo wa kuongoza pale wapewapo nafasi, hivyo anaomba apatiwe hiyo nafasi ili watu waone atakacho kifanya.