watu walio tembelea leo

Rachel Njigo: Mitingo ya kiasili ya Kitanzania itaivusha Tanzania kimataifa!

Msanii na mwanamitingo Rachel Njingo akiwa amebeba kibuyu cha maji.

Msanii na mwanamitindo na mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Rachel Bitulo Njingo ‘Tausi wa kitanzania ’ amesema ili Tanzania ijitangaze kimataifa ni vema ikageukia mitindo na kuachana na sanaa nyingine za kimagaribi. Akizungumza na mwandishi wa habari hivi Paskal Mgundu wa http://bestmoviesartist.blogspot.com/ kwa njia ya simu mojakwamoja toka Dodoma nchini Tanzania,  Njingo amesema mitindo ya kiasili ndiyo sanaa pekee nchini ambayo inaweza kukubalika kimataifa kama mavazi ya kimasai, kisukuma,kigogo nk. 'Tumeshindwa kwenye sanaa nyingine ikiwemo urembo lakini tutaitumia vema mitindo basi tunaweza kuitangaza Tanzania kimataifa', amesema. Njingo ambaye ni mwanamitindo kupitia kampuni ya Makeke Modelling iliyo jijini Dar es salaam ya nchini Tanzania ametamba kuwa Tanzania ina vivutio vingi vitakaoweza kuitangaza