
Mmiliki wa wimbo bora wa Hip Hop 2015 kwa mujibu KTMA Prof Jay, ameanza kuweka wazi mipango yake na “plan” zake za kutatua changamoto kadhaa kama atafanikiwa kushinda Ubunge mwaka huu.
Akizungumza kupitia kipindi cha “The jump off” cha Times fm, Prof amefunguka changamoto ya kwanza atakayoifanyia kazi kwa upande wa wasanii kuwa ataonganisha umoja wa wasanii.
“Nitapambana kuleta umoja wetu, unajua sisi wasanii hatuna umoja sasa nitasimamia kushikamana kuleta umoja huu ili hata tukiiambia Serikali kuhusu Pirates tuwe na nguvu moja sio huyu anayake na huyu pia yuko na yake yani kila mmoja analia na kilio chake sasa inabidi tuwe na sauti moja.” Alisema Jay
Prof amekiri kupata ushindani katika mbio hizo kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba, ila anaamini malengo yake ya kuwatumikia wananchi pamoja na sera nzuri za chama chake vitamfanya kulinyakua jimbo hilo.