watu walio tembelea leo

Nisha: Huyu ‘Malaika’ Aliniambia “Mama Nibebe”


Nisha: Huyu ‘Malaika’ Aliniambia “Mama Nibebe”
  • Nisha: Huyu ‘Malaika’ Aliniambia “Mama Nibebe” 1
Tangaza nasi bure ....
Tembelea : 

Nisha: Huyu ‘Malaika’ Aliniambia “Mama Nibebe”

Huyu malaika alinambia mama inama nikwambie,nikainama kumsikiliza

Akanambia "mama nibebe"
Nilimnyanyua na kumuweka mapajani mwangu,akanilalia mabegani mwangu

Wengine walikuwa wanaendelea kuftari ila nakumbuka mm nilishindwa kuftari nikimfikiria huyu mtoto wa miaka 4-5 kwanini kaninong'oneza mama nibebe??? Nimejifunza upendo,watoto hawa wanahitaji mapenzi yetu sisi tulioko nje.
Wakiwa nasi wanafarijika sana,hata usipowapa chochote just mapenzi na kuwajali wanafarijika,maskini kammiss mommy yake

Zamani nilivyokuwa nasoma nikigombana na mtu akinambia maziwa kama unanyonyesha watoto yatima nilikuwa nakasirika sana,ila now natamani ningekuwa na uwezo wa kumnyonyesha kila aliyekosa maziwa ya mama yake, kumbeba kila aliyetamani mikono ya wazazi wake,kumfuta machozi kila anayejihisi yuko peke yake

Huwezi kunielewa kama hujapitia haya,ila kama unanielewa anza kusaidia wenye kuhitaji msaada wako sasa.
Nishabebee on instagram
Hongera sana Nisha kwa moyo wako huo wakujitoa.