watu walio tembelea leo

Batarokota : Sitakurupuka Kugombea Udiwani!


Pichani kutoka kushoto msanii Batarokoa, aliyekuwa kocha wa Taifa staa Maxio Maxino na Stevini Shija meneja kampeni wa Batarokoa
Tembelea : www.batarokota.blogspot.com
Staa wa Bongo Bongo fleva na nyimbo za asili ya kitanzania  na aliyeingia kwenye tuzo za KTMA 2014 katika katengoli ya Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania, Paskal Linda Mgundu ‘Batarokota’ ambaye mwezi julai atatangaza nia yake ya kugombe udiwani mwaka huu wa uchaguzi amedai kua hatakurupuka kuutaka udiwani kupitia kata ya Tungi  mkoani Morogoro na kuwa ataendeleza sanaa hata akiwa diwani.
Akizungumza na Kiss fm jijini Nairobi jana alisema..’Kwanza ninataka kuwahakikishia washabiki wangu sitakurupuka, nimekuwa  mwanachama wa chama cha Mapinduzi  umoja wa vijana almost miaka 5  lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 1 tawi la gome ya ushindi , nimekuwa mwamasishaji  wa chama cha mapinduzi kwa nyimbo na sanaa kwa muda mrefu.
Kwa hiyo nataka kusema sitakurupuka na wala sitatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu Fulani amegombea na mimi basi tu  nigombee hapana  nimeona  katika kata yangu ya  tungi kuna matatizo kadhaa  nani anaweza kuyatetea hayo matatiizo  basi mimi ndio nitakuwa mtetezi wa kata pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za mziki asili na bongo fleva nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za udiwani’alisema